Friday, June 15, 2012

Fina Mango ajiandaa kurudi hewani


Wale waliokuwa wameimiss sauti ya mtangazaji wa zamani wa kipindi cha Power Breakfast Fina Mambo wana haki ya kuyaanda masikio yao tena kuipokea sauti yake tamu itakayoanza kusikika tena kwenye mawimbi ya radio.
Kwa mujibu wa interview ndefu aliyoyafanya na mtandao wa ‘Bongo Celebrity’ Fina amesema fununu za kwamba anafungua radio station yake mwenyewe si za kweli japo hewani atarejea kwa nguvu mpya kwakuwa amewamiss sana pia wasikilizaji wake.
“Hapana sio radio yangu mwenyewe. Masoud yupo hewani tayari Times FM na ninatumaini kufanya mambo yangu kwingine pia….. Nipo kwenye maandalizi ya mwisho, so sooon!
Kwa muda mrefu Fina ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Bernard Joseph,amekuwa akiendelea na kazi kwenye kampuni yake mwenyewe iitwayo 1Plus Communication,yeye akiwa mkurugenzi mtendaji.
Kampuni yake inayokua kwa kasi nchini inahusika na masuala ya mawasiliano ya umma kwa niaba ya makampuni makubwa , matangazo, uandaaji wa matukio na mambo mengine.
Kuhusu kufanikiwa katika kazi za makampuni kama hayo, Fina anasema, “Unahitaji kujuana na watu, unahitaji kuelewa namna mambo yanavyofanywa, yakubali na endana nayo haraka. Pia unatakiwa kuwa na hela ya kutosha na kuweza kumudu uingiaji wako wa pesa.Malipo yanaweza kuchelewa hata kwa siku 60 kama una bahati mbaya kihivyo, kazi zinaendelea na unahitaji kuwa na hela kuendelea kufanya kazi.Hata hivyo soko hili bado changa sana, mengi yanahitajika na mengine bado yanaweza kufanyika.”
Kuhusu uoga wa baadhi ya wajasiriamali wanaohofia kuanza kwakuwa hawana wazo la biashara mpya, Fina anasema, “Nadhani wajasiriamali huwazaliwa kuwa hivyo na hutengenezwa pia. Kinachohitajika ni mchanganyiko wa shule, mafunzo na uzoefu wa kazi ili kukupa uwezo wa kuanza na kuendelea.
Kwa wale wanaoogopa kuanza, basi huenda haukumaanishwa kuwa mjasiriamali na kama ukilazimisha uko hatarini kuchanganyikiwa. Ushauri wangu endelea kuajiriwa kwakuwa wote hatuwezi kuwa wajasiriamali. Kama hauna wazo la pekee la biashara, usilazimishe.”

No comments:

Post a Comment