Tuesday, April 24, 2012

Solange Agoma Kurekodi na Beyonce

Mdogo wa Mwimabji nyota Beyonce, amesema hawezi kurekodi muziki na dada yake kwa sababu wako tofauti sana. Katika Interview aliyofanya na Complex magazine ya Marekni Solange ambaye humsaidia dada yake kuandika baadhi ya nyimbo anazorekodi kama ‘Get me Bodied na ‘Why Dont you love me’ amesema yeye na Bey wako tofauti sana kimuziki na hivyo hata personality zao ziko tofauti na haitanoga wakirekodi pamoja. Solange ambaye ni DJ wa muziki, anakaa Brooklyn NY na mtoto wake mmoja wa kiume ana utofauti hata wa muonekano na Beyonce na anatarajia kuachia album yake karibuni pamoja na designs za nguo.

No comments:

Post a Comment