Tuesday, February 21, 2012

NAVAA SUTI ZENYE THAMANI YA SH, LAKI 5 KILA MOJA – BANANA ZORRO…!!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Banana Zorro, amesema kuwa katika suala la mavazi, mara nyingi huwa ananunua nguo zenye gharama kubwa ambapo suti zote anazomiliki kila moja amenunua kwa shilingi laki 500,000.
Akizungumza na DarTalk, msanii huyo alisema hana tatizo la fedha hivyo kutoa kiasi hicho cha pesa haoni tatizo kwani anahitaji kupendeza muda wote.
Alisema huwa anafanya manunuzi ya nguo kwa mwezi mara tatu, na kila anapoenda dukani hutumia shilingi milioni 10, hadi kumaliza mahitaji yake yote ikiwa pamoja na yale ya familia.
“Najipenda sana na ndiyo maana navaa nguo za bei mbaya, siyo kwamba ninajisifia lakni huo ndo ukweli uliyopo, unajua maisha haya ukiwa hutumii pesa huwezi kuendelea au kufanya chochote cha maana,” alisema.

No comments:

Post a Comment