Tuesday, June 12, 2012

Listen and download A New P-Square Track Feat Rick Ross-Beautifu Onyinye

Jana remix ya video ya P-Square imesambaa kwenye internet. Hata hivyo kwa upande wa video iliyowekwa YouTube sasa hivi huwezi kuiona kwakua imeondolewa kutokana na masuala ya kisheria. Kama umeenda kuiangalia YouTube basi bila shaka ulipoicheza ukakutana na maneno haya, "This video is no longer available due to a copyright claim by Iroko Partners Ltd.Sorry about that." Hata hivyo video hiyo bado inapatikana kwenye website zingine za kuhifadhia video. Kwanza kabisa kama kuipa mic basi sisi hii ngoma tumeipa tano kabisa. Ukiisikiliza 'Beautiful Oyinye' unaweza ukaifananisha kidogo na 'No One Like You' hasa kwa jinsi drums zinavyopiga. Mwanzoni Rick Ross anasikika akiwapa shavu mapacha hao 'P-Square' kisha akaipa shavu Konvict Music kabla ya ID yake maarufu ya 'Maybach Music' na ngoma inaanza kudunda. Pengine pamoja na P-Square kuzikamua poa verse zao wengi walitaka wasikie Rick Ross atatambaa vp kwenye beat hiyo ya Kiafrika. Rick Rozay amethibitisha kuwa ni rapper anayebadilika muda wowote kutokana na mazingira na kwakweli karap poa sana. Tunatabiri hii ngoma itafanya vizuri sana pengine usishangae kama ikiipita Chop my money!

No comments:

Post a Comment