Wednesday, June 13, 2012
Kwanini Beyonce alimpa mwanae jina la Blue Ivy?
Tangu ijulikane kuwa Beyoncé na Jay-Z wamemuita mtoto wao wa kwanza Blue Ivy watu wamekuwa wakijaribu kutafuta maana halisi ya jina la binti yao. Kuna wale waliofikiri kuwa limetokana na mapenzi ya Jay-Z kwa rangi ya Blue, lakini Bey ameandika shairi ambalo huenda likawa na sababu halisi ya kwanini waliamua kumuita binti yao Blue.
“Dunia ni ya blue katika ncha na kina chake. Blue hii ni rangi iliyopotea. Mwanga katika kikomo cha mkusanyiko wa rangi hausafiri umbali wote kutoka kwenye jua kuja kwetu. Hupotea miongoni mwa ‘molecules’ za hewa na kusambaa kwenye maji. Maji hayana rangi, maji ya juu huonekana kuwa na rangi ya chochote kilichopo juu yake, lakini maji ya kina huchukua rangi zote zilizosambaa, maji yakiwa halisi zaidi ndivyo huwa na rangi ya blue zaidi.”
Ujumbe huo kutoka kwenye kitabu cha mwandishi Rebecca Solnit kiitwacho ‘Field Guide to Getting Lost’ uliandikwa na Beyoncé kwenye blog yake ya mtandao wa Tumblr jana.
Kabla ya Beyonce kujifungua watu walijaribu kubashiri jina la mtoto wao ambapo watu walidhani angeitwa Brooklyn (kutokana na mstari maarufu wa Jay-Z “If we had a daughter, guess what I’m a call her? Brooklyn Carter), Sasha, Babyonce n.k.
Baada ya kujulikana kwa jina alilopewa mtoto wao kuna watu wakalihusianisha jina Blue Ivy na “Eulb Yvi”, wakidai kuwa lilikuwa jina la Latin la binti wa Lucifer (shetani) na mjadala ukaibuka kwenye mtandao wa Twitter.
Mtandao wa The Examiner ukapuuzia dhana hiyo kwa kusema Biblia haijataja kama Lucifer ana mtoto wa kike na hakuna jina Eulb Yvi kwenye kamusi ya kilatin. (Fun fact: Unajua kuwa ni marufuku kumuita mtoto wako Lucifer nchini New Zealand?)
Kulikuwepo pia na mitazamo ya maana kuhusiana na uchaguzi wa jina hilo. Good Morning America walidai kuwa Ivy ni utani wa numerali IV ya Roma. Namba nne ni muhimu kwa wanandoa hao – walifunga ndoa April 4, (4/4), siku zao za kuzaliwa ni tarahe 4 (September na December), na albam ya nne ya Beyonce ilipewa jina la “4.” (Huffington Post).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment