Tuesday, June 12, 2012
JACKIE Chandiru wa Uganda Achaguliwa Kufungua Show ya Sisqo
Mwananadada Jackie Chandiru amekuwa msichana pekee atakayefungua show ya Sisqo, mwezi August mjini Kampala Uganda ambapo ataungana na Jose Chameleone na rais wa Ghetto, Bobi Wine.
Mapromoter wa show hiyo Chinedu Ikoroha na Misairi Kabira wamemchagua Jackie na kuwamwaga Iryn Namubiru, Juliana Kanyomozi, na Keko baada ya kuonekana kuwa uwezo wake ni mkubwa katika stage.
Jackie Chandiru ni mwanamuziki wa zamani wa kundi Blu3 ambapo tangu mwaka 2010 amekuwa na mafanikio makubwa kama solo artist.
Tayari ameshasaini mkataba na sasa anasuburi show hiyo ya mwanamuziki wa kundi la Druhill Sisqo aliyetamba na vibao kama Thong Song, Unleash the Dragon na Incomplete.
Show ya Sisqo itafanyika kwenye uwanja wa Kyadondo Rugby tarehe 25, August 2012.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment